Hhhhmm!
Ah! Leo chereko chereko
Mwanenu nimekuwa
Zile kuringa mideko itapungua

Ahsante mama ulinifunza nkajua
Baba kasema kuomba mwiko
Raha ya chumvi kununua

Tena si kwa nazi
Si hirizi za waganga
Kwa baraka za baba na mama
Tu na dua

Waambie paparazi
Pingamizi wenye viranga
Waliosema hayawi hayawi yamekuwa
Ooh! Oh!

Iyena Iyena
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Kwaheri tutaonana

Iyena Iyena (aah ooh)
Iyena Iyena (aah Iyeena)
Iyena Iyena
Ntawakumbuka sana

Ooh! Ndoa baraka
Ukipata ushukuru
Maana wanayoililia ni wengi sana
Kwetu talaka
Kuitoa ni kufuru
Nimefunzwa vumilia
Niushinde ujana

Ili kesho mahususi
Kusudi wasinong'one
Embu nichumu niringe washushuke
Na hii pete ya harusi
Nakuvisha waone
Wakale sumu
Wavimbe wapasuke

Eeh!
Ati nashika nanga
Nteke nsichomoke ndani (anameremeta)
Futa namba wablock vimada wa zamani (anameremeta)
Sio vijembe vya kanga waziwazi mambo hadharani (anameremeta)
Waliopanga mwenye nyumba kaja ndani (anameremeta)

Iyena Iyena (aah iyoyo)
Iyena Iyena (aah Eeeh)
Iyena Iyena
Kwaheri tutaonana (oh! Kwaheri baba mama)

Iyena Iyena (Iyeeena)
Iyena Iyena (aah eeh)
Iyena Iyena
Ntawakumbuka sana

Imefika tamati
Tulisubiri kitambo
Leo samaki
Kanasa kwenye chambo

Pongezi kwa kamati
Yanavutia mapambo
Napata picha safi
Litanikoma bundle

Mwanamke usafi
Gaga kulisugua
Mume akirudi sharti
Viatu kumvua
Kitandani marashi
Massage kumchua
Kisha anza sayansi
Viuno kutengua

Mambo ya kuzima taa
Si mahaba ni kuwanga
Washa japo ka mshumaa
Mumeo aone shanga

Eeeeh!
Makeup kinanda
Kaka suit kama mbunge (anameremeta)
Mulo changa muda kujipooza na punje (anameremeta)
Momo ndani Shivo amekuja na Fumbwe (kanameremeta)
Kula chanda ukishiba ruksa kafunge (anameremeta)

Iyena Iyena (ah iyeee)
Iyena Iyena (ah iyoyo)
Iyena Iyena
Kwaheri tutaonana (eh! Kwaheri baba mama)

Iyena Iyena (Iyeee)
Iyena Iyena (hhmm)
Iyena Iyena
Ntawakumbuka sana

Saa nataka kusasambua (sasambu)
Me nasasambua (sasambu)
Aby Dad nasasambua mimi (sasambu)
Sasambua!
Tuone

Mguu moja juu (sasambu)
Usishushe chini (sasambu)
Cheza jitazame (Sasambu)
Sasambua!
Tuone

Aisha kimobitel (sasambu)
Nipe za baloteli (sasambu)
Nyonga kibaiskeli (sasambu)
Sasambua!
Tuone

Akaa kama unashika ukuta (sasambu)
Ifanye unashusha (sasambu)
Taratibu zungusha (sasambu)
Sasambua
Tuone

Sasambu! Sasambu! Sasambu!
Sasambua!
Tuone

Kama unawasha bajaji (sasambu)
Imwagie na maji (sasambu)
Tuwakomeshe vizazi (sasambu)
Sasambua!
Tuone